Mwandishi huyu wa habari anahitaji Msaada wako Kuokoa Maisha yake

Wanahabari Hellena Mwango, Careen , Kulwa Mwaibale na mke wa Patrick Mwillongo wakiwa wamekaa nje ya jengo la Hospitali ya Mkoa Temeke wakitafakari namna ya kumsaidia Mwillongo walipofika  kumjulia hali leo hii asubuhi.

Na Mwandishi Wetu

Ndugu wanahabari mwenzetu Patrick Mwillongo yupo hoi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ambako amelazwa kwa matibabu.

Mwillongo anasumbuliwa na ugonjwa wa kujaa maji kwenye mapafu ambao umesababisha hashindwe kujimudu kufanya jambo lolote.

Kwa umoja wetu na tabia tuliojijengea kama wanahabari tujitokeze kumsaidia mwenzetu ambaye anapita katika kipindi kigumu.

Mwillongo ni Mwandishi wa Habari wa kujitegemea
 na anafanya shughuli zake wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na awali alikuwa akiandikia magazeti mbalimbali likiwemo Jambo Leo na yale yanayomilikiwa na Kampuni ya New Habari.

Kwa atakayeguswa kumsaidia anaweza kutoa mchango wake kupitia namba MPESA-0754362990, Tigo Pesa ni 0712727062


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo