WAZIRI Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amewaongoza mamia ya wakazi wa Dar es salaam kuuaga mwili wa mwanasiasa wa muda mrefu, Richard Tamilway maarufu kwa jina la ‘Tambwe Hiza’ aliyefariki dunia alihamisi Februari 8, 2018 nyumbani kwake Mbagala Kizuini na kuzikwa leo katika Makaburi ya Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) akiwemo Katibu mkuu wa Chama hicho, Vincent Mashinji na mke wa Mh Lowassa, Regina Lowassa wameshiriki katika shughuli hiyo.
Vingozi wengine wa chama hicho walioshiriki msiba huo ni pamoja na Meya wa jiji la Dar, Isaya Mwita, Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, Godbless Lema, Peter Msigwa na wengine wengi.
Akimwelezea marehemu Hizza, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amesema msiba huo ni pigo kwa chama hicho na kwamba taifa limempoteza mwanasiasa machachari.
Hiza anafahamika sana kwa siasa zake akiwa chama cha wananchi (CUF), Baadae alihamia chama cha mapinduzi (CCM) na akiwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda 2015 aliamua kuondoka CCM na kuhamia CHADEMA.
Marehemu Tambwe Hizza amezaliwa mwaka 1959 na amefariki Dunia Februari 8 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 59. Marehemu ameacha wajane wawili na watoto kadhaa.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina.