Mchungaji aliyemzalisha mwanafunzi akamatwe kabla ya kesho Jumapili

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuagiza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa kumtia mbaroni kiongozi wa dini (mchungaji) anayedaiwa kuzaa watoto wawili na mwanafunzi aitwaye Selina, kisha kumtelekeza.

Makonda ameyasema hayo leo wakati Feb. 10, 2018 wakati akitatua kero za wananchi wa Dar es Salaam alipokuwa akifanya mkutano nao katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar na alipoagiza mchungaji huyo akamatwe kabla ya kesho Jumapili.

“Jambo moja limenifedhehesha, naomba RPC Salum Hamdani umjulishe Lazaro Mambosasa, namhitaji huyu mchungaji aliyekatisha ndoto za huyu mwanafunzi na kumpa ujauzito mara mbili. Amefika akaomba msaada akamrubuni akampa mimba, amerudi tena amempa mimba ya pili. Mtu tunayemtegemea atupeleke mbinguni anatupeleka motoni, hawa ni mawakala wa shetani.

“Tumeona yaliyotokea kwa ‘Nabii Tito’ anapiga pombe huku anatembea na Mke na mfanyakazi, hana hata aibu, kuna watu wanalitukanisha jina la Kristo, wanajitangaza kuwa Watumishi wa MUNGU kumbe ni Washetani, watu wa namna hii tusiwavumilie turipoti kwenye mamlaka mapema.

“Ameshampa mimba mwanafunzi halafu anapata wapi ujasili wa kusema BWANA YESU ASIFIWE? Nataka akamatwe kabla ya Jumapili kufika, ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Makonda.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo