Kutokana na umuhimu wa mwanafunzi kupata chakula shuleni, wakati mwingine huwalazimu walimu kutoa gharama zao wenyewe kuwanunulia chakula wanafunzi ambao wazazi wao hawajachanga fedha ya chakula
Hayo yamesemwa na Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Ikonda Enerika Kayombo na kusema yeye ni mmojawapo wa mwalimu ambaye amekuwa akitoa gharama zake kuhakikisha wanafunzi ambao hawajachangiwa chakula na wazazi wanapata chakula
"wakati wenzao waliochanga wanakula chakula, ambao hawajachanga unakuta wanakuwepo eneo wanapopata chakula wenzao, unawafukuza lakini wakati mwingine inakulazimu kugharamia ili wale, binafsi nimefanya hivyo, kamati ya shule ni mashahidi" amesema mwalimu huyo
