Mahakama Yawaachia Mbunge Sugu na Masonga

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya leo Februari 10, 2018 ameamuru washtakiwa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga kuachiwa kwa dhamana ya milioni tano kwa kila mmoja

Kufuatia maaamuzi ya mahakama hiyo kesi inayowakabili Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga itasikilizwa tena Februari 26, 2018 
Sugu na Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Pombe Magufuli wanayodaiwa kuitoa Desemba 30,2017 na sasa washatakiwa hao wanatetewa na Wakili Msomi Peter Kibatala


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo