Mahakama Tanzania sasa kwenda kidijitali

Serikali ya Tanzania kupitia Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amesema hawaitaji tena kuendelea kupata aibu katika kuendesha kesi ndani ya Mahakama zilipo nchini kwani kwa sasa watatumia mfumo mpya wa tehama kuhifadhi jalada mbalimbali

Profesa Ibrahimu Juma ameeleza hayo leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama yaliyofanyika jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa Rais John Magufuli na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi.
"Mahakama imejiwekea malengo ya kuongeza uwazi na ufanisi katika masuala ya utawala na uendeshaji wa mashauri na tehama tumeona ndio jibu sahihi kwa Mahakama karne ya 21 inayolenga kuwa na uwazi pamoja na ufanisi...
Mahakama hatuhitaji tena aibu ambazo zimezoeleka za jalada zilizopotea au halionekani, hatuhitaji hadithi ya jalada linahitaji kufutwa vumbi kwanza au stakabadhi ya malipo ya shughuli haionekani, hatutaki kusikia mteja shauli lake liko wapi, kwa nani na ni lini au lipo mbele ya Jaji yupi", alisema Profesa Ibrahimu Juma.
Pamoja na hayo, Jaji Mkuu aliendelea kwa kusema "tumepanga kufuta hayo yote ili kujenga historia mpya katika msingi wa tehama, tumeadhimia na hatutaki kubaki nyumba na tutaendelea na kasi ya mabadiliko ya kunufaika kutokana na mafanikio makubwa ya tehama tumelenga kuyashuhudia na kunufaika na manufaa ya tehama kwenye eneo la usimamizi wa fedha, ukosaji wa takwimu, mapato, usikilizaji wa mashauri".
Kwa upande mwingine, Profesa Ibrahimu Juma amemkumbusha Rais Magufuli lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kuanzisha Mahakama zinazotembea ili kuweza kuwafikia popote walipo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo