Ni tukio lililojiri mapema Leo jtatu Feb 5, katika kikao cha baraza LA madiwani wa Jiji la Arusha ,pale askari kanzu wa Polisi walipovamia baraza hilo wakisaka nyaraka ya siri inayodaiwa kupatikana kwa mmoja wa madiwani wa baraza hilo.
Askari hao walifika na kufunga lango la ukumbi wa mikutano huku wakizuia madiwani hao kutoka kwa lengo la kuwafanyia upekuzi wakisaka nyaraka ya serikali inayodaiwa kumilikiwa na Diwani mmoja wapo, Prosper Msofe(chadema)
Jambo hilo linadaiwa kuwafedhehesha na kuwadhalilisha madiwani wa kike ambao waliwaeleza wanahabari kuwa askari hao hao hawakuwatendea haki kwa kuwa kitendo hicho cha kupekuwa pochi zao kilipaswa kufanywa na askari wa kike jambo ambalo halikufanyika hivyo.
Mmoja wa madiwani hao ,Veronica Hosea Mwilange alisema kitendo hicho kimewadhalilisha wao kama madiwani wa kike
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia akiongea wakati akitoka kwenye ukumbi huobwa mikutano alisikika akisema askari huwa hawafundishwi kazi ya kufanya.
Hata hivyo baada ya upekuzi huo uliochukua takribani dakika 30 ,askari hao waliondoka na Diwani Msofe kwa ajili ya mahojiano Polisi baada ya kudai kuwa anayo nyaraka inayoonyesha Meya wa Jiji na mkurugenzi wamesaini mkataba wa maduka ya stand ndogo na wafanyabiashara kinyume na maazimio ya baraza hilo