Polisi walivyomchukua Diwani wa CHADEMA Arusha

February 5, 2018 baadhi ya Madiwani wa CHADEMA katika Halmashauri ya Jiji la Arusha wamesusia na kutoka nje ya ukumbi wa Halmashauri wakati wa kuapishwa kwa Madiwani Wapya wawili waliochaguliwa kupitia Chama cha Mapinduzi kwa madai ya kupinga walivyochaguliwa.
Baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza la Madiwani, Jeshi la Polisi Arusha limemshikilia Diwani wa Kata ya Daraja Mbili Prosper Msofe kwa madai ya kukutwa na Nyaraka za siri za serikali.

Msofe ametiwa mbaroni na jeshi la polisi akiwa katika kikao cha baraza la madiwani kilichokuwa kikifanyika katikabukumbi wa baraza hilo mapema leo akituhumiwa kumiliki nyaraka za siri za halamashauri hiyo.

Tukio hilo ambalo limewaduwaza madiwani waliokuwa kwenye baraza hilo ,limetokea majira ya saa 11 Jioni baada ya askari polisi takribani 8 wakiwemo waliovalia kiraia kuvamia ukumbi wa mikutano na kuanza kufanya upekuzi kwenye mikoba ya madiwani hao ikiwemo ya kike wakisaka nyaraka hizo .

Hata hivyo mara baada ya kukamilisha zoezi la upekuzi waliondoka na diwani huyo  kwa kumpakia kwenye  gari lenye namba PT 1222 aina ya landrover.


Msofe alipatikana na dhahama hiyo mara baada ya kumtuhumu mkurugenzi wa jiji pamoja na meya wa jiji  kusaini mkataba na wafanyabiashara wa maduka eneo la stand ndogo kinyume na maazimio ya baraza hilo na kuonyesha nyaraka iliyosainiwa jambo lililosababisha mkurugenzi kuhoji upatikanaji wa nyaraka hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo