Mh. Iyombe ameyasema hayo leo wakati akizungumza na watendaji na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, ambapo amesema kwamba kuchukua maamuzi hayo ambayo hayajafanyiwa utafiti wa kina kwani yanaleta athari kiutendaji na kisaikolojia kwa watumishi.
Mbali na hayo Kiongozi huyo akizungumzia migogoro ya ardhi mkoani humo amedai kwamba mingi imekuwa ikisababishwa na baadhi ya watendaji kwa kutotimiza wajibu wao ipasavyo hasa suala la sheria na taratibu za nchi.
Mhandisi Iyombe amesema, wapo watendaji ambao wanashindwa kutumia Mamlaka waliyopewa ili kuzuia migogoro ya ardhi, na kwamba, migogoro mingi inaanzia sehemu wanazotwaa ardhi ili kupima kwa kuwasilisha taarifa zilizo na mapungufu.