Mwanaume huyo ambaye alikuwa akifanya biashara ya mitumba katika eneo hilo, amefanya tukio hilo asubuhi ya Jumapili hii huku akiaacha ujumbe kwa watu wake wa karibu wamwambie mke wake huyo awaangalie watoto.
“Aliniambia ankwenda mbali na kuniomba nimwambie mama Sharon awaangalie watoto wake kwa ajili yake, ahtukujua akimaanisha kifo”, amesema Bi. Tabitha Bernad ambaye ni mkwe wa marehemu Wambua.
Mkwe wake huyo ameendelea kwa kusema kwamba mara nyingi marehemu alikuwa akimlalamikia kuwa mke wake ana tabia ya kuleta wanaume tofauti tofauti nyumbani kwao na kulala nao, iliniumiza kwa kweli lakini hatukupata muda wakuzungumza zaidi”, amesema Bi. Tabitha ambaye pia ni mkwe wa marehemu.