CCM yaigomea Taarifa Ya DC Makete


 Mbunge wa Jimboo la Makete Mh Prof Norman Siggala

 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete akionesha taarifa hiyo iliyokataliwa


Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Mh Veronica Kessy ameshindwa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi (CCM) iliyotakiwa kuwasilishwa leo katika kikao cha Halmashauri ya CCM wilaya.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mh Kessy amesema ameshindwa kusoma taarifa hiyo kutokana na mapungufu aliyoyaona kwenye taarifa hiyo, ambayo amekabidhiwa hii leo na ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri

Amesema awali alitakiwa kukabidhiwa taarifa hiyo tangu jumatatu ya wiki hii kama alivyoagiza, na badala yake akakabidhiwa Jumanne na alipokwenda kuipitia aliikuta ina mapungufu makubwa, na kuagiza yarekebishwe lakini alipokabidhiwa ameikuta pia inamapungufu yaliyopelekea  kutoiwasilisha

Mkuu huyo amesema kutokana na taarifa hiyo kutowasilishwa kama ilivyopangwa, wote waliosababisha taarifa hiyo kuwa na mapungufu watawajibika kuitisha kikao kingine kwa gharama zao huku wakitakiwa kuiandaa upya taarifa hiyo

Hali hiyo ikamfanya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Ndugu Ona Nkwama, kuagiza taarifa hiyo ikaandaliwe upya huku akiwaonya watendaji wa halmashauri, kuepuka kuzembea utakelezaji wa shughuli mbalimbali ambazo zinapelekea kuandaliwa kwa taarifa ambayo haijitoshelezi kuwasilishwa kwenye kikao


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa, amesema kwa kuwa taarifa hiyo haijaandaliwa na baraza kama mamlaka ya nidhamu ya watumishi hao itafuatilia kwa makini na kubaini kama kuna sababu zozote za uzembe zilizofanywa na miongoni mwa watumishi hawa

Katibu wa CCM wilaya ya Makete Langael Akyoo ametoa kauli kuhusiana na suala hilo kwa kusema kuwa taarifa hiyo ikaletwe upya


Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Makete Francis Namaumbo amekiri kwenda kuyatendea kazi maagizo yote aliyopewa

 Wajumbe hao




JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo