Breaking News: Diwani wa CHADEMA Auawa kwa Kukatwa Mapanga Morogoro

Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Namwawala wilaya ya Kilombero Godfrey Luena ameuwawa kwa kukatwa katwa na mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo

Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje- CHADEMA John Mrema na kusema ni kweli Diwani wao ameuliwa akiwa nyumbani kwake jana (Alhamisi).
"Ni taarifa za kweli aliuwawa jana Luena majira ya saa 1 usiku kwa kukatwa katwa mapanga akiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana. Mpaka sasa hatujaelewa chanzo cha kifo chake kwa kuwa kilitokea usiku lakini tumekwisha toa taarifa kwa Jeshi la Polisi na walienda eneo la tukio wakasema watafuatilia", amesema Mrema.
Kwa upande mwingine, Mrema amesema kama chama bado wanafuatilia tukio hilo kwa ukaribu ili waweze kubaini chanzo cha tukio hilo ni nini pamoja na aliyehusika na mauaji hayo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo