Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Mkoa wa Iringa Godfrey
Nyang'oro ameachiwa kwa dhamana leo baada ya kushikiliwa kwa saa kadhaa na jeshi la
polisi
Mwandishi huyo amekamatwa na jeshi la polisi katika
viwanja vya Mahakama mkoani Iringa na kupelekwa Kituo cha polisi mjini Iringa
kwa mahojiano zaidi
Akizungumza nasi kuhusu tukio hilo, Katibu wa chama cha
waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Tukuswiga Mwaisumbe amesema
mwanahabari huyo amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kupiga picha mahakamani
wakati shughuli za mahakama zikiendelea
Amesema picha hizo zilipigwa na kusambazwa kwenye
mitandao ya kijamii wakati shughuli za mahakama zikiendelea jambo ambalo
limekanushwa na mwandishi huyo baada ya kuhojiwa na polisi na kudai kuwa yeye
alipiga picha kabla ya shughuli za mahakama kuanza
Amesema jeshi la polisi limemuachia kwa dhamana huku
likishikilia simu zake kwa uchunguzi zaidi ambapo huwenda leo jeshi hilo
linatarajiwa kutoa maamuzi baada ya kumhoji
Sikiliza mahojiano hayo hapo chini>>>>>>