Basi la abiria Kampuni ya Fikoshi Investment linayofanya safari zake kati ya Bukoba na jijini Mwanza limepata ajali katika eneo la Nkwenda Wilayani Kyerwa mkoani Kagera, na kusababisha kifo cha kondakta wa basi hilo
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Agustine Ollomi , amesema ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva na kutokuwa na ufahamu mzuri wa njia hiyo kutokana na ugeni.
Katika ajali hiyo kondakta wa basi hilo ambaye bado hajafahamika jina lake, alifariki papo hapo, huku majeruhi kadhaa wamekimbizwa katika hospitali ya Nyakahanga, na wengine katika Kituo cha afya Nkwenda kilicho karibu na eneo la ajali.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi