Yupo Hoi Hospitalini baada ya kung'atwa na Paka

MVULANA kutoka kijiji cha Ngaani, Kaunti ya Tharaka-Nithi, amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kaunti ya Nyeri baada ya kushambuliwa na paka mwitu

Wavulana wengine watatu wanatibiwa katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Chuka.

Akizungumza na wanahabari, mmoja wa viongozi wa kijiji Bi Josphine Ciambaka alisema kwamba mwanafunzi huyo alishambuliwa alipokuwa akirejea nyumbani jioni kutoka shuleni.

Alihamishwa hadi hospitali ya Nyeri kwa matibabu zaidi. “Mvulana huyo aliumwa na paka mwitu na kujeruhiwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili wake,” alisema Bi Ciambaka.
Alisema paka huyo amekuwa akiwashambulia watu wanaotembea kwenye barabara hiyo na amekuwa hatari kwa wanafunzi wa shule za kutwa ambao wanahitajika kutembea kila asubuhi na jioni.
Bw Patrick Murithi, mmoja wa waathiriwa walioshambuliwa Ijumaa alimuona paka huyo akimjia kwa ukali akamrukia na kumshambulia huku akimuacha na majeraha mabaya sehemu mbalimbali mwilini.
“Paka huyo hutoa sauti isiyo ya kawaida anapomuona mtu wala haogopi hata watu wazima,” Bw Murithi alieleza. 
Bw Julius Mutegi alisema wazazi wamelazimika kuwasindikiza wanao hadi shuleni asubuhi na kuwachukua jioni huku baadhi ya wanafunzi wakiamua kukaa nyumbani kwa kuogopa kushambuliwa.
Wameomba serikali kuingilia kati na kumuua paka huyo mwitu ambaye wamekuwa wakiwinda kwa mapanga na mishale bila mafanikio yoyote kwa siku tatu zilizopita.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo