Wakati Mahakama mbalimbali nchini zikiendelea kufanya tofauti tofauti kwa jamii kuelekea kilele cha wiki ya sheria nchini, mahakama ya mwanzo Lupalilo wilaya ya Makete Mkoani Njombe imetoa elimu ya masuala ya sheria kwa wananchi wake
Hii leo wanafunzi wa shule ya sekondari Lupalilo wilayani Makete Mkoani Njombe wamepatiwa elimu ya masuala mbalimbali ya sheria, ikiwemo ufanyaji kazi wa mahakama zote nchini, mahakama za watoto, mirathi migogoro ya ardhi pamoja na kuruhusu maswali kwa wanafunzi hao kuhusu masuala ya kisheria
Kilele cha siku ya sheria nchini huadhimishwa Februari Mosi ya kila Mwaka
Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya Mwanzo Lupalilo James Sikazwe akitoa elimu kwa wanafunzi Lupalilo sekondari
Wanafunzi wakiuliza maswali ya ufahamu
Wanafunzi wakisikiliza elimu hiyo
Hakimu mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Lupalilo Mh. James Edwin Sikazwe akitoa elimu kwa wanafunzi hao













