Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kongwa White Zuberi wakati kikao cha baraza la madiwani lilofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo na kusema vitabu hivyo walikabidhiwa kwa ajili ya kukusanyia mapato mbalimbali ili waweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana na kukaidi amri halali ya mkurugenzi.
"Vitabu hivyo vimetolewa kutokana na kuwapo kwa idadi ndogo ya mashine za kielektroniki ambazo zipo 64 na maeneo mengine kukosa mashine hizo na halmashauri kuamua kutumia vitabu halali 95 vya kukusanyia mapato lakini mpaka sasa 15 havijarejeshwa", alisema Mwenyekiti.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi amewataka watendaji wa kata, vijiji, maafisa elimu na walimu kuacha kuwachangisha wazazi kuhusu elimu bali iwapo wazazi wamechanga lazima wawasilishe kwa mkurugenzi.
