Wavunja kanisa na kuiba

Watu wasiojulikana wamevunja kufuli ya mlango wa Kanisa la Baraka na Uzima (GRM) lililopo Mtaa wa Kokehogoma Kata ya Turwa wilayani Tarime, na kufanikiwa kuiba vitu mbali mbali vilivyomo ndani

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Henry Mwaibambe, amesema waumini wa kanisa hilo hawakugundua mpaka Mchungaji wao alivyokuja na kugundua kuna vitu havipo, na ndipo ilipobainika kuwa watu hao wameiba jenereta, spika pamoja na viti.
“Mimi nimepata taarifa mtaani lakini baadaye zikafikishwa ofisini kwangu, na taarifa zilizopo ni kwamba wameiba jenereta moja, spika moja na viti vya plastiki vya kukalia, sasa waumini walipoingia kanisani hawakugundua mpaka mchungaji alipoingia ndio akagundua kuna vitu vimepungua, kwa haraka haraka thamani yake haiwezi kufika milioni nne”, amesema Kamanda Mwaibambe.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaibambe amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana na jeshi la polisi linawasaka wahusika wa tukio hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo