Rais Magufuli amesema hayo akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 8, 2018 wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Madini ambapo Rais Magufuli amesema tayari ameshamuagiza Waziri Mkuu kuhakikisha mtu anayehusika na kupeleka mbolea anafanya hivyo na kama asipofanya hivyo aachie ngazi.
"Napozungumza hapa ipo mikoa ambayo haijapelekewa mbolea moja wapo ni mkoa wa Rukwa. Wakati tunazungumzia 'The Big four' kwa ajili ya uzalishaji wa chakula lakini mbolea bado hazijapelekwa lakini Waziri wa Kilimo yupo na kwenye bajeti alipitisha sasa nimeshatoa maagizo kwa Waziri Mkuu kwamba mbolea zisipofika huko ndani ya wiki hii huyo anayehusika na kupeleka mbolea aachie ngazi" alisema Rais Magufuli
Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa " Labda tukianza kufukuzana pengine tutajifunza, nilishasema wale wote niliowateua mimi wasifikiri ni sherehe bali wanakuja kufanya kazi na mtu ambaye nitakuwa namteua anafikiri hawezi kufanya kazi asikubali uteuzi wangu na uteuzi wangu nataka tukatatue matatizo ya Watanzania"