Nicolaus Tulusi (36) aliyekuwa anatumia madawa ya kulevya aina ya Heroin toka mwaka 1987 akiwa darasa la 4.
Akizungumza kwa uchungu mkubwa kijana wa miaka 36 anayeitwa Nicolaus Tulusi ambaye ameanza kutumia madawa ya kulevya toka akiwa darasa la nne, amesema chanzo cha yeye kuendelea kutumia madawa baada ya kumaliza shule na kukosa kazi ya kufanya.
Nicolus ameacha kutumia madawa miaka miwili na nusu iliyopita, lakini madawa hayo yamemsababishia madhara makubwa kama kutokuwa na nguvu ya kufikiria kama awali, kuumwa mwili, kutokua na nguvu ya kufanya kazi vyema.
“Nawashauri vijana wenzangu waache kutumia madawa ya kulevya kwani ni hatari sana na yanapunguza muono wa kufanya maendeleo, maana kijana wa sasa anatakiwa na maendeleo na sio kutumia madawa ya kulevya,” alisema Tulusi.
Diwani
wa Kata ya Temeke Shaban Msombo akifafanua juu ya serikali kuwasaidia
vijana walioathirika na madawa ya kulevya hapa nchini.
Kwa upande wake Diwani Kata ya Temeke Shaban Msombo alisema kuwa, vijana hao wanapewa ushauri wa jinsi gani ya kujitambua juu ya kuacha kutumia madawa ya kulevya, kwa sababu biashara ya madawa ya kulevya ni kubwa na inafanywa na watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha na hivyo kusababisha kuwa na kipindi kigumu kuzuia biashara hiyo isifanyike.
Tunaiomba sana serikali iendelee kuwasaidia vijana walioathirika na madawa hayo.
Leo ni siku ya maadhimisho ya kimataifa ya madawa ya kulevya kitaifa inafanyika Mkoa wa Mbeya katika viwanja vya Nzovwe, mgeni rasmi ni Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal.
Ujumbe wa mwaka kuhusu madawa ya kulevya: “Uteja wa dawa za kulevya, Unazuilika na kutibika. Chukua hatua.”
Chanzo:Taarifa news