Diwani wa Kata ya Kimara ktk Wilaya ya Ubungo, Paschal Manota amejivua udiwani na uanachama wa CHADEMA katika barua aliyoandika Januari 20 mwaka huu.
Katika barua yake ameainisha sababu kadhaa ikiwemo kuwepo kwa kutofautiana kati yake na Meya wa wilaya hiyo.
Sababu nyingine ni Meya kuita wanachama wa CHADEMA takataka, kukosa ushirikiano toka chamani na madai ya kushinda uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji lakini ushindi kupewa mtu mwingine.
=======
Siku chache baada ya kuandika barua hiyo, Bw. Manota leo(Januari 27) ameonekana kwenye ufunguzi wa Kampeni za CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo Jimbo la Kinondoni ambapo amekabidhiwa rasmi kadi ya CCM.
