Nape: Nasema wenzetu watasubiri sana kwani haiwezekani kuiangusha CCM madarakani"

Mbunge wa jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye amefunguka na kusema upinzani nchini Tanzania hautaweza hata siku moja kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika madaraka kwa kuwa inapofika wakati wa kutafuta dola hawana urafiki na mtu

Nape Nnauye amesema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombe ubunge wa jimbo la Longido kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ambao unatarajiwa kufanyika kesho Januari 13, 2018.  
"Ikifika wakati wa kutafuta dola CCM inakuwa kitu kingine kabisa, unaweza kuichezea wakati wa kawaida na tunaweza kupiga stori ila ikifika kwenye kutafuta dola hapo ni mambo mengine kabisa. Ndiyo maana nasema wenzetu watasubiri sana kwani haiwezekani kuiangusha CCM madarakani" alisisitiza Nape Nnauye


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo