Picha za ambulensi hiyo ikipakiwa mbao zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku zikizua malalamishi kutoka kwa wakaazi wa Isiolo na wakenya kwa ujumla.
Dkt Kuti alisema kwamba alipata habari kumhusu dereva huyo kupitia mitandao ya kijamii.
“Nimepokea malalamishi kutoka kwa raia kuwa mshukiwa huyo amekuwa akiitisha hongo ili kuwahudumia wagonjwa wanaotaka huduma ya ambulensi hiyo. Huu ni utumizi mbaya wa mamlaka na ni ufisadi ambao sitauvumilia,” alisema Dkt Kuti.
Aliwaonya madereva wa magari ya kaunti hiyo kuwa watachukuliwa hatua kali iwapo watapatikana wakitumia mali hiyo ya umma (magari) vibaya au kujinufaisha nazo.
Dkt Kuti vile vile alisikitika kuwa madereva wamekuwa wakitumia magari ya serikali kwa njia isiyofaa.
Alisema kuwa serikali yake itaunda idara maalumu itakaysimamia masuala ya usafiri wa magari ya kaunti hiyo.
Baada ya kuchukua hatua hiyo, wakaazi wa Isiolo walimpongeza gavana huyo. Aliwasifu raia kwa kufichua habari hiyo na kuwarai waendelee kutoa maelezo watakapogundua yasiyowapendeza.
“Mnastahili pongezi. Tusaidieni kwa kufichua maovu ili mpate huduma bora zaidi,” akasema.