Charlote ambaye alikuwa akimtumia rafiki yake meseji kwa kutumia snapchat akimwambia kuwa amelala na mwanaume mwengine, alikosea kutuma meseji hiyo na kwenda kwa mpenzi wake Jack Hurst mwenye umri wa miaka 20.
Watu wa karibu wa wawili hao wamesema kwamba baada ya kufanya hivyo alimtumia meseji ya kumuomba radhi Jack na kumuaga ikisema ..”Kwa heri, tafadhali nisamehe, nakupenda, lakini kujua kuwa unanichukia inatosha”.
Baada ya hapo Jack alianza kumtafuta kwenye simu mpenzi wake huyo bila mafanikio na kuamua kuita polisi na kwenda chuoni kwao kumtafuta, na kukuta amejinyonga karibu na eneo la chuo alichokuwa akisomea masuala ya afya.
Jack Hurst ambaye ni mpenzi wa Charlote
