Mtulia leo kupitia mtandao wake wa kijamii amesema kuwa anawapenda sana watu wa Kinondoni na kusema yupo tayari kuwatumikia tena kwa kuwapa maendeleo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
"Kwaza, nawasalimu wote na khasa wananchi wenzangu wa jimbo la Kinondoni. Nawapa pole sana kwa maumivu makali mliyoyapata kutokana na uamuzi wangu wa kujiuzulu ubunge wa jimbo letu la Kinondoni kupitia chama cha CUF. Nawahakikishia kwamba bado nawapenda sana na niko tayari kuwatumikia tena kwa lengo la kuleta Maendeleo kwenye jimbo letu" aliandika Mtulia
Mtulia alitumia nafasi hiyo kutangaza nia yake kutaka kugombea "Nichukie fursa hii kutangaza nia kwa wanakinondoni wote na Watanzania kwa ujumla kuwa nitachukua form ya kuomba ridhaa kwenye chama changu cha CCM na endapo chama changu kitaridhia basi nitakuja mbele yenu kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya ubunge wa jimbo letu Kinondoni"
Kufuatia ujumbe huo ndipo hapo baadhi ya wananchi walianza kumpa maneno wakionyesha hisia zao juu ya jambo alilofanya na analotaka kulifanya.