Diwani wa Donyomurwak kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, Lwite Ndossi amejiuzulu nafasi yake na kujivua uanachama wake katika chama hicho na kijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amethibitisha hilo na kusema kuwa wamempokea diwani huyo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kupoteza baadhi ya viongozi wake katika ngazi mbalimbali ambao wamekuwa wakijiuzulu nafasi zao na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile wanachosema wanaunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake