Wananchi wa kata ya
Lupalilo wilayani makete mkoani Njombe ambao watoto wao wamefaulu kuendelea na
kidato cha kwanza Januari 2018, wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanaripoti
shuleni walikopangiwa
Akizungumza kwenye
mkutano wa hadhara wa kijiji cha Mago, diwani wa kata hiyo Mh. Imani Mahenge
amesema suala hilo sio la hiari, hivyo wazazi watumie muda huu kufanya
maandalizi ya watoto wao mapema ili kusiwe na visingizio vya kutowapeleka shule
watoto wao
Amesema kwa sasa
tayari Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Makete ameshampatia orodha inayoonesha
wanafunzi wote wa kata ya Lupalilo waliohitimu darasa la saba na kufaulu na
shule ambazo wamepangiwa kwenda, na kwa kuwa ni jukumu la kata kusimamia watoto
hao wapelekwe shuleni, amewataka wazazi wote kutekeleza agizo hilo
Angalia video hii hapa chini:-