Waandaji wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, Kampuni ya Lino International Agency Limited, wamesema kwamba hakutakuwa na Fainali za Taifa za shindano la Miss Tanzania kwa mwaka 2017
Katika taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo leo imeeleza kuwa sababu kubwa ya kuahirishwa kwa shindano hilo ni ukosefu wa Wadhamini ambao kwa njia moja au nyingine huwezesha kufanyika kwa mashindano hayo kwa kulipa gharama mbalimbali ikiwemo zawadi za washiriki.
Aidha waandaaji hao pia wamesema kuwa kuchelewa kupata kibali cha kuanza mchakato wa Miss Tanzania 2017, ambacho kilitolewa na BASATA mwezi Septemba mwaka huu pia kimechangia kukosa kwasababu muda ulikuwa umeshaenda.
Mashindano ya kutafuta warembo wa Miss Tanzania yamekuwa yakifanyika kila mwaka na baadae kuibua mastaa mbalimbali kama Wema Sepetu, Lulu Diva, Jokate Mwegelo na wengine wengi.