Tundu Lissu awapa tumaini Watanzania

Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu amewatoa hofu Watanzania juu ya afya yake kwa kusema kuwa hali yake inaendelea kuimarika.
Akielezea hali yake, Mhe. Tundu Lissu amesema kwa sasa anauwezo wa kukaa bila kuegemea kwenye kitu chochote, hali ambayo awali alikuwa anashindwa kufanya hivyo.
Ninawashukuru kwa sala na maombi yenu. Sasa ninaweza kukaa bila ya kuegemea kitu.“ameandika Mhe. Lissu kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Juzi Jumanne Desemba 26, 2017 Mhe. Lissu alisimama kwa mara ya kwanza kwa msaada wa Madaktari baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mnamo mwezi Septemba 7, 2017 mjini Dodoma.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo