Mwili wa mwanajeshi mwengine aliyeuwawa Congo kuwasili kesho

Mwili wa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Marehemu SGT Issa Saleh Issa aliyekuwa majeruhi akipatiwa matibabu nchini Uganda baada ya shambulio la Waasi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo utawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Terminal I kesho saa 6:00 mchana.
Marehemu SGT Issa Saleh Issa alikuwa katika Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini DRC.
Baada ya kuwasili kwa maiti hiyo, itapelekwa moja kwa moja Kijijini kwao Ndijani Wilaya ya Kati Mkoa Kusini Unguja kwa mazishi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo