TFF Yapiga marufuku mashindano yoyote ya soka yaliyo nje ya mfumo

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amefuta mashindano yoyote ya soka yaliyo nje ya mfumo wa shirikisho hilo isipokuwa tu kwa kibali maalum

Karia ameyasema hayo leo katika Mkutano wake na Wahariri wa vyombo vya habari ambapo amesema mashindano ya soka yasiyo rasmi kama ambayo huandaliwa na wanasiasa majimboni na hata na baadhi ya taasisi na wadau, yamekuwa yakipewa umuhimu mkubwa kuliko mashindano rasmi ya TFF zikiwemo ligi.
“Wakati umefika sasa Wabunge na wanasiasa kwa ujumla watoe fedha kuzidhamini timu za majimboni mwao badala ya kuanzisha mashindano ya ng’ombe na mbuzi”, amesema Karia.
Pamoja na hilo lakini Rais Karia leo amesaini mkataba wa udhamini wa jezi za timu zote za taifa zikiwemo za vijana na wakubwa kwa wanawake na wanaume. Mkataba huo unathamani ya zaidi ya Sh. Milioni 800.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo