Rais Magufuli leo amesaini nyaraka za wafungwa aliowasamehe jana

Rais John Magufuli leo ametia saini nyaraka za msamaha alioutoa kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza Viking (Babu Seya ) na Johnson Nguza (Papii Kocha ) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela

Rais ametia saini nyaraka hizo Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Msamaha huo aliutoa jana Jumamosi Desemba 9,2017 katika maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara). Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kazi nzuri ya kurekebisha tabia za wafungwa.
Taarifa ya Ikulu imesema Rais Magufuli amesisitiza kuwa pamoja na kutolewa msamaha huo, vyombo vya dola viendelee kusimamia sheria.
Nimeona nitumie kifungu hiki cha Katiba - Ibara ya 45 (1) ambacho nilipewa na Watanzania, ingawa kilikuwa hakijawahi kutumika, unajua mtu ambaye alihukumiwa kunyongwa halafu baadaye anaachiwa, ni kitu kinashangaza kwa sababu hakijawahi kutokea, lakini nimeona nifanye hivyo kwa ajili ya Watanzania,” amesema.
Ameongeza, “Muendelee kusimamia wajibu wenu na kusimamia sheria, mtu anayehukumiwa kufungwa afungwe kweli, na nilishatoa wito kwa magereza, pasiwepo wafungwa wa kukaa tu na kupumzika, wafanye kazi, kufungwa si kustarehe.”
Akizungumzia hilo, Kamishna Jenerali wa Magereza Dk Juma Malewa amemshukuru Rais kwa kutoa msamaha huo wa kihistoria.
Amesema wafungwa na maofisa Magereza wameipongeza hatua hiyo ambayo itasaidia kuwatia moyo wafungwa wanaorekebishwa tabia katika magereza nchini na kuongeza kwamba wafungwa waliopatiwa msamaha wa kuachiwa huru, waliruhusiwa kutoka magerezani tangu jana.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo