Rais Magufuli awajaza walimu mapesa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendesha harambee na kuchangisha jumla ya milioni 60 ambazo watapewa wajumbe wa Chama Cha Walimu ambao wamehudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu CWT

Rais Magufuli alianzisha zoezi hilo kwa kutoa milioni 10 ili wajumbe hao waweze kupata fedha za chakula na baadaye Rais kuanza kuwaita viongozi mbalimbali wa Serikali na taasisi za Serikali ili waweze kuchangia fedha za chakula ambapo kwa ujumla ziliweza kupatikana jumla ya milioni 60.
Katika zoezi hilo la uchagiaji wa fedha hizo za chakula kwa wajumbe 1200 wa CWT lilikuwa kama ifuatavyo
Rais Magufuli milioni 10
Waziri Mkuu  Milioni 10 
Waziri wa Elimu, Ndalichako milioni 6
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama  milioni 6 
Mama Magufuli Milioni 1
Mama Majaliwa  Milioni 1 
Spika wa Bunge Job Ndugai Milioni 5 
Katibu Mkuu Tamisemi Milioni 4
Naibu Katibu Mkuu Tamisemi  Milioni 4
Mstahiki Meya wa Dodoma Milioni 1 
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Milioni 1
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mstaafu) George Mkuchika Milioni 3 
Mkuu wa Chuo cha Dodoma Milioni 4 
Mkurugenzi wa usalama wa taifa Milioni 4 
Jumla ya fedha zilizopatikana zilikuwa milioni 60 hivyo Rais Magufuli aliagiza kuwa milioni 50 wapewe wajumbe wa CWT huku milioni 10 zikienda kwa walimu wanafunzi wa UDOM ambao walishiriki katika Mkutano huo. Lakini pia Rais Magufuli aliagiza fedha hizo zifike kabla ya wajumbe hao hawajamaliza Mkutano wao. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo