Rais Dkt John Magufuli amesema endapo akifariki dunia hataki kuzikwa Dodoma na badala yake atazikwa alipozikwa baba yake Chato Mkoani Geita
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Mkoani Dodoma wakati akizindua mradi wa nyumba zilizojengwa na shirika la nyumba la taifa (NHC)
Amesema ameshawauliza viongozi wakiwemo marais wastaafu ambao wamesema nao wakifa wanataka wakazikwe walikozaliwa, hivyo hakuna atakayetaka kuzikwa mkoani Dodoma katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kuwazika viongozi wa serikali
"Yani mimi nikifa nizikwe hapa kwa Wagogo? waje wakacheze na fisi kwenye kaburi langu? Haiwezekani, hapa labda Mzee Malecela na Mh Spika, naye spika amesema atazikwa Kongwa nyumbani kwake" amesema rais Magufuli
Hata hivyo Rais Magufuli ameagiza eneo lililotengwa kwa ajili ya kuzikia viongozi mkoani Dodoma Lirudishwe kwa wananchi walitumie
