Msamaha wa Rais Magufuli waua Mtu

Ikiwa ni siku chache zimepita mara baada ya msanii mkongwe Nguza Viking maarufu kwa jina la Babu Seya na mwanae Papii Kocha kuachiwa huru kutokana na kupewa msamaha wa rais Magufuli katika sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika Desemba 9, mwaka huu mjini Dodoma familia hiyo imepata pigo baada ya mdogo wa Babu Seya aitwaye Crizo Chimbukizi kufariki dunia.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia hiyo, King Kikii, Crizo alifariki dunia jana kutokana na mshtuko wa moyo baada ya kupewa taarifa ya kuachiliwa huru kwa wawili hao na kwamba taratibu za mazishi zinafanywa.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa mkoa wa Katanga Kongo nyumbani kwa familia ya Nguza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli alitoa msamaha kwa mwanamuziki maarufu Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Jonson Nguza maarufu kama Papii Kocha wasanii waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo