Waziri Jafo ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake Wilayani Muheza ambapo alikagua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Alisema Mradi huo kwas asa umefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake na Mkandarasi umeahidi hapa mbele ya wananchi kwamba utaukamilisha ndani ya muda niliokupa ambao ni wiki sita kuanzia hivi sasa.
“Sitegemei kuskia sababu zozote zitakazofanya mradi huu usikamilike ndani ya wiki sita ni mategemeo yangu wananchi wataanza kufaidi matunda ya mradi huu baada ya muda mfupi tu kuanzia sasa, Mkandarasi fanya kazi yako” Alisema Jafo.
Katika ziara hiyo Waziri Jafo amefanikiwa kutembelea Miradi ya afya na elimu katika kituo cha afya Mkuzi na Ubwari pamoja na kutembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kilulu.
Waziri Jafo amewapongeza wadau mbalimbali wanaoshirikiana na Serikali katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Maeneo ya Umma. Hususan ni Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI) kwa kutoa mifuko 50 ya Saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miundombinu katika kituo cha Afya Ubwari.
Halkadhalika Waziri Jafo ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha ajenda ya maendeleo kwa wananchi.
Tamisemi ya Wananchi.