Mwananchi akichangia hoja
Mwananchi Aldoline Sanga akichangia hoja kwenye mkutano huo
Diwani wa kata ya LupaliloMh Imani Mahenge akizungumza kwenye mkutano huo
Wananchi wa kijiji
cha Mago wilayani Makete mkoani Njombe wameukataa mradi wa maji uliokusudiwa
kupelekwa kijijini hapo na serikali
Wakizungumza kwenye
mkutano wa hadhara kijijini hapo hii leo wananchi hao wamesema hakuna tatizo la
maji katika kijiji chao kwa sasa, hivyo mradi huo wa maji upelekwe kwenye
vijiji vingine vyenye uhitaji wa maji huku wakimtaka diwani wao kuwapigania
maendeleo ya shughuli nyingine kijijini hapo ikiwemo barabara
Diwani wa kata ya
Lupalilo Mh. Imani Mahenge ambaye ameshiriki mkutano huo awali ametumia fursa
hiyo kuwaelewesha wananchi ujio wa mradi huo kabla ya wananchi hao kuamua
kuukataa
Baadhi ya wananchi
wametoa maoni yao kuwa kijiji hicho kina maji mengi, hivyo kwa sasa shughuli za
maendeleo nyingine zipewe kipaumbele ambazo ni barabara, zahanati pamoja na
ujenzi wa darasa la awali katika shule ya msingi Mago
Baada ya majadiliano
na maamuzi ya wananchi, diwani Mh Mahenge akawashukuru wananchi na kuwaomba
wawe na moyo wa kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo kijijini hapo
Sikiliza sauti zao hapo chini:-