Mbunge John Mnyika ajitoa

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amejitoa na kuwaombea askari 14 wa JWTZ ambao wamefariki dunia nchini Congo wakati wakilinda amani huku askari wengine 44 wakiwa wamejeruhiwa

Mbunge wa Kibamba ameitumia Jumapili ya leo Disemba 10,2017  kuwaombea mashujaa hao na kuwapa pole wanafamilia wote ambao ndugu zao wamepoteza maisha katika tukio hilo.
"Kwa kipekee naitoa ibada ya leo kuwaombea Mashujaa wetu,askari 14 wa JWTZ waliojitoa mhanga na maisha yao kuitetea amani Congo, 44 ambao wamejeruhiwa na wale wawili (2) ambao hawajulikani walipo. Mungu awajalie pumziko jema kwa wale waliopoteza uhai kupigania amani"
Mnyika aliendelea kusema kuwa 
"Awape uponyaji majeruhi na kusaidia kupatikana kwa Askari wawili. Aijalie faraja na ustawi familia za wahanga na wote ambao wameguswa kwa moja kwa moja au namna ingine yeyote na tukio baya hilo" aliandika John Mnyika 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo