Akizungumza na wana-CCM waliohudhuria mkutano mkuu ambao ulifanya uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti wa chama hiko Taifa, Jakaya Kikwete amesema alipata ugumu kumtetea Magufuli kwa sababu kwenye wasifu wake hakuwa kushika wadhifa wowote ndani ya chama hiko, na kuhofia huenda akashindwa kuongoza.
"Tulipokuwa kwenye mchakato, moja ya kazi kubwa nilikuwa nayo kama mwenyekiti ni kutetea kwamba Magufuli anafaa, na hoja mojawapo ni kwamba hajawahi hata kuwa balozi wa nyumba kumi, hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa shina, atawezaje kuwa mwenyekiti, anatoka tu paaap kuwa mwenyekiti wa taifa", amesema Jakaya Kikwete.
Hapo jana Rais Magufuli amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kupata kura zote halali 1821.