Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema ameonesha masikitiko yake baada ya taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kutupilia mbali ushahidi wa video walioupeleka ukionesha viongozi waliojiuzulu (madiwani) wakipokea rushwa
Kupitia Ukurasa wake wa Twitter Mbunge Lema amesema kesho Jumatatu atazungumza na waandishi wa habari kuhusu suala hilo
Angalia hapa chini alichokiandika Lema
Kuna vitu ambayo Mume hawezi kumfanyia au kumsaidia mke wake hata kama anampenda kwa dhati sana ,kwa mfano kubeba mimba. Ndivyo ambavyo ni dhahiri kwa Takukuru kuhusu suala la Madiwani walionunuliwa. Nitaongea na vyombo vya habari kesho— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) December 17, 2017