Wananchi walaani Bar inayozalisha wabakaji huko Zanzibar

Wananchi wa Shehiya ya Kiomba mvua Wilaya ya kaskazini B  wahofia maisha yao  kutokana na  uwepo wa baa ya mabatini  inachangia kuongezeka vitendo viovu ikiwemo vya wizi na ubakaji katika maeneo yao.
Wakizungumza  nje ya Mahakama  ya Wilaya ya Mfenesini Katibu wa Sheha Shehia hiyo Semeni Juma Nyange na baadhi ya wananchi  wamesema  hali  ya usalama wao  umekuwa hatarini  tokea kuwepo kwa baa hiyo kwani  vijana wengi wanao jihusisha na ulevi  hutumia  shehia hiyo kufanyia mambo yao maovu ikiwemo wizi,uhalifu wa aina mbalimbali.
Wamesema  wamekuwa  wanashindwa kufanya shughuli zao za kijamii  kutokana walevi wakisha lewa hujifisha kwenye mapori na kutishia  kuwabaka wanawake na watoto wanao kwenda kutafuta kuni.
Wakizungumzia hatua walizozichukua ili  baa hiyo iondoshwe wamesema  malalamiko  yao waliyafikisha katika ngazi mbalimbali ikiwemo  ngazi ya shehia,Wilaya hadi Mkoa  lakini bado halijafanyiwa ufumbuzi hivyo wameiomba mahakama ya vileo  kutowapa   kikali  wamiliki wa baa hivyo  kwa mwaka  2018 ili kunusuru vizazi vyao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo