SUMATRA: Marufuku abiria kuzungumza siasa, dini, biashara ndani ya basi


MAMLAKA YA Usimamizi wausafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) imepiga marufuku abiria kuzungumza masuala ya siasa, dini na kufanya biashara wawapo safarini.

Agizo hilo limetangazwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Lingadi Ngewe na kwamba abiria atakayebainika kufanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Agizo hilo linakuja baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwapo kwa mvutano wa kupinga kanuni mpya kati ya Sumatra na chama cha wamiliki mabasi yaendayo mikoani (TABOA) na wa usafiri Dar es Salaam (UWAMADAR).

Bila kutaja ni sheria na kanuni ipi, Mkurugenzi huyo amesema ufanyaji wa vitendo hivyo katika mabasi ni kinyume na kanuni za usafirishaji.

"Tutaanza kuzuia wasafiri wa wapo ndani ya mabasi kuacha kuzungumza masuala ya siasa, dini na kufanya biashara. Tukibaini hilo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa abiria na dereva ikibidi," amesema na kuongeza

‘Kwa madereva hasa wa kwenda mikoani, njiani wanapandisha wafanyabiashara na kufanya biashara ndani ya basi, hatua kali zitachukuliwa kwa dereva na huyo anayefanya biashara.’


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo