Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani amesema Tume hiyo haijavizuia vyama vya siasa kufanya kampeni kwenye kata zenye uchaguzi mdogo wa madiwani.
Kailima amesema hayo jijini Dar Es Salaam na kuvitaka vyama vya siasa kunadi sera na ilani zao katika muda uliopangwa na eneo husika lenye uchaguzi tu.
Uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 unatarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu.