Jumla ya baa kumi na nne za Wilaya ya Mjini leo zimefika katika mahakama ya Vileo Zanzibar Mwanakwerekwe kwa ajili ya kuomba kibali cha kuendeshea biashara ya Vileo kwa mwaka 2018.
Akizungumza nasi Mwenyekiti wa Mahakama ya Vileo Zanzibar Mohammed Subeit amesema amepokea maombi kumi na nne ya wamiliki wa mabaa kwa ajili ya kuendesha shughuli za vileo katika maeneo yao ya biashara.
Aidha amesema ni muda muwafaka sasa kwa wananchi wa Wilaya ya mjini kufika mahakamani kwa ajili ya upingaji wa maombi hao kama kuna baa zinazoleta usumbufu kwao ikiwemo kupiga miziki kwa sauti kubwa,zilizopo katika makaadhi ya wananchi,na zile zisizofata sheria kwa wananchi.
Hata hivyo Subeit amesema endapo hakutakuwa na wapingaji kwa baa hizo na mahakama ikajiridhisha kisheria basi hakutakuwa na sababu kwa baa hizo kunyimwa kibali kwa ajili ya kuendesha biashara ya vileo.
Na:Amina Omar.
