Mahakama yatupilia mbali Kesi ya Mwanamuziki Diamond Platnum


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto imeitupilia mbali kesi  iliyofunguliwa na Mwanamitindo Hamisa Mobeto dhidi ya Mwanamuzi Diamond  Platnum. 

Uamuzi huo umetolewa leo Novemba 10/2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa mahakama hiyo. 

Hakimu Devotha alitoa uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika kutokana na msanii Diamond kuwasilisha pingamizi dhidi ya kesi  hiyo iliyofunguliwa na Mobeto. 

Katika pingamizi lililowasilishwa na Diamond mahakamani hapo anadai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa  kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto. 

Awali Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine  alikuwa anaomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond. 

Mwanamitindo huyo alifungua kesi hiyo mahakamani hapo akiiomba mambo  mbalimbali likiwemo la matunzo ya mtoto waliozaa na msanii huyo. 

Katika kesi hiyo, Hamisa anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya  mtoto ya kila mwezi. Hamisa alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake  Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century 
Attorneys. 

Kupitia hati hiyo ya madai, mwanamitindo huyo anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia  yake. 

Hata hivyo, Diamond aliwasilisha hati ya majibu kinzani  akipinga maombi hayo ya Diamond akidai gharama anazodai kulipwa kwa  mwezi sh. milioni tano kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi  kuzimudu. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo