Madiwani jimbo la Mbowe kuhamia CCM

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Humphrey Polepole, amesema kuwa nusu ya madiwani kwenye baraza la madiwani la halmashauri ya Hai waliomba kuhamia CCM

Polepole ameyasema hayo leo wakati akitoa tathmini ya uchaguzi mdogo wa madiwani, uliofanyika Novemba 26 kwenye kata 43 ndani ya mikoa 19 nchini.
Amedai kuwa Madiwani hao kutoka jimbo hilo ambalo mbunge wake ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe waliomba kuhamia CCM wakati ambao viongozi wa CCM walipopita kufanya tathmini ya hali ya kisiasa jimboni hapo.
“Tulipita pale Hai kipindi fulani ambapo ndio Moyo wa chama kikuu cha upinzani na wakatuomba sana karibu nusu ya baraza la madiwani kwenye halmashauri wahamie CCM lakini tukaona si vizuri wote waondoke”, amesema Polepole. Ameongeza kuwa waliwaambia wahamie kwa awamu ambapo walianza na mwenyekiti wa halmashauri kisha kufuatiwa na madiwani wengine wawili.
CCM imeibuka na ushindi katika kata zote tatu zilizofanya uchaguzi Wilayani Hai ambazo ni Mnadani, Machame Magharibi na Weruweru. Katika matokeo ya jumla CCM imeibuka na ushindi katika kata 42 kati ya 43 zilizofanya uchaguzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo