Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa (kulia) akitangaza mabadiliko hayo katika baraza la madiwani
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Mwl. Gregory Emannuel akizungumza jambo kuhusu mabadiliko hayo katika baraza hilo
Baraza la Madiwani Halmashauri ya
wilaya ya Makete mkoani Njombe baada ya kupokea kero kutoka kwa wananchi,
limekubali kufanya marekebisho ya sheria ya utozaji ushuru wa mbao kwa wilaya ya
Makete
Hayo yamebainika katika Baraza la
Halmashauri hiyo lililoketi hapo jana ambapo maamuzi hayo yamezingatia maoni
mengi yaliyokuwa yakitolewa na wananchi kuhusu sheria hiyo
Mwanasheria wa Halmashauri Bw.
Godfrey Gogadi ndiye aliyetoa taarifa ya Marekebisho hayo kwenye baraza la
madiwani ambapo amesema ni jambo la kawaida kwa sheria kufanyiwa marekebisho na hakuna kosa lolote hapo na baadaye baada ya majadiliano na wajumbe wa baraza hilo maamuzi yakatangazwa na mwenyekiti wa halmashauri Mh Egnatio
Mtawa
Akitangaza mabadiliko hayo Mh Mtawa amesema awali ushuru wa mbao uliokuwa unatozwa sh. 250 kwa ubao mmoja sasa utatozwa sh 150 kwa mbao laini na sh. 250 kwa mbao ngumu kuanzia alhamisi ya Novemba 23 huku akiagiza wataalamu wa halmashauri wanaohusika na mashine za kielektroniki za kutoza mapato wabadilishe viwango hivyo katika mashine zote
Sikiliza zaidi kwa kubofya play hapo chini:-