CCM yaviburuza Vibaya vyama vya upinzani

Chama cha mapinduzi CCM kimeibuka na ushindi katika kata 42 kati ya 43 zilizofanya uchaguzi mdogo wa udiwani jumapili ya Novemba 26 kwenye mikoa 19 nchini

Hayo yamebainishwa leo na katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Ndugu Humphrey Polepole, wakati akitoa tathmini ya uchaguzi mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo ya makao makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es salaam.
Polepole amesema kuwa Chama chake kimeibuka na ushindi huo katika kata hizo ikiwa ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya CCM.
Polepole ameitaja kata ambayo chama chake kimekosa ushindi kuwa ni Ibigi iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya ambayo imechukuliwa na mgombea wa CHADEMA. Aidha Polepole amedai kuwa chama kimeumia kwa kuikosa kata hiyo lakini kimekubali matokeo.
Kwa upande mwingine Polepole amezitaka mamlaka kushughulikia haraka baadhi ya dosari zilizojitokeza kwenye baadhi ya maeneo, ambayo chama hicho kimeripoti kutoridhishwa na mwenendo wa mchakato wa uchaguzi ikiwemo vitendo vya vurugu vilivyofanywa na watu wasiokuwa na nia njema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo