Wengine Watu watatu wafa maji Ziwa Victoria

Watu watatu wamefariki dunia Ziwa Victoria katika Kisiwa cha Ilamba wilayani Muleba Mkoani Kagera baada ya mtumbwi wao kuzama. Watu hao walikuwa wakitoka kuchota maji Kisiwa cha Mazinga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema watu hao walizama jana Jumatatu saa 6:30 mchana, ambapo mwili Adela Andrea (26), mkazi wa Kijiji cha Itongo umeopolewa na Nelson Boniphace (20), mkazi wa Kisiwa cha Ilamba aliogelea na kuokolewa.
Kamanda Olomi amesema, miili ambayo haijapatikana ni ya Superius Severine (27) mkazi wa Kijiji cha Nyakitaba na Evelius Zephrine (22) mkazi wa Mubunda Kitoko wilayani Muleba
Olomi amesema mtumbwi huo uliokuwa na madumu 33 ya maji amesema unamilikiwa na Rashidi Sabini (33), mkazi wa Kijiji cha Ilamba na kwamba ulizama baada ya kupigwa na mawimbi kutokana na upepo mkali


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo