Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wilbroad Mtafungwa amesema kuwa, jeshi la polisi litaendelea kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya kuwepo na watu wanaomiliki silaha ili wazisalimishe, sehemu yoyote.
Aidha katika hatua nyingine kamanda Wilbroad Mtafungwa amesema kuwa, kufuatia matukio ya vijana waliokuwa wameibuka na vitendo vya kuwapora wasafiri, na katika nyumba za kulala wageni, jeshi hilo limefanikiwa kuwatia mbaroni vijana 11, maarufu wa wakiwemo pamoja na wengine watano wenye mtandao wa wizi wa pikipiki mkoani Tabora